Mdau akiwa katika pozi la kutokea! kitaani kwao mitaa ya Ilala! sio Masaki tu pazuri hata Ilala panatisha! hebu tazama hiyo background yake!!! usipaiiimeee! weeeee! achaaa hizo!.
Thursday, May 21, 2009
HATA DESIGN TUNAWEZA SIYO UTANGAZAJI TU!
HAPO VIPI!!!! WE MWENYEWE SI UNAONA SMILE HILI! KAMA VIPI TUNAWEZA KUKUTANA KUPITIA E-MALI YANGU YA mashauzi@gmail.com. KWA PAMBA NA VIPODOZI VILIVYOENDA SKONGA....
DU HATA WEWE? HII INATISHA
Spika wa bunge la wanafunzi wa uandishi wa habari DSJ akiwa katika kibanda kimoja cha mama ntiliye aliyefahamika kwa jina moja tu la mama Manka! akitoka kuchukua maandazi kwa ajili ya kwenda kupata kifungua kinywa kabla ya safari ya kwenda kutembelea sehemu moja ya kihistoria ifahamikayo kama KINUKAMORI WATER FALLS, Sasa swali na hofu yangu ni kwamba je! alikuwa anakula peke yake au aliokuwa na wenzake mh! jamaniiiii!
“NAPENDA NINI”-JAFARAI
Enzi zile alipoanza kutambulika rasmi ilitokana na wimbo wake uliokwenda kwa jina “Nipo Bize”.Si unakumbuka jinsi alivyokuwa akimwambia kimwana wake kwamba asimtafute kwa sababu yuko bize?
Basi yawezekana ni kweli kwamba mshkaji huwa yuko bize kwani Jafarai ameshakamilisha albamu yake mpya itakayokwenda kwa jina Wali Nazi. Albamu hiyo itakuwa na nyimbo 9 ambazo zote zimerekodiwa katika studio za Fish Club za jijini Dar.Katika albamu hiyo Jafarai amewashirikisha wasanii wengine kama vile mwanadada Naazizi kutoka Kenya,Lamar ambaye pia ni producer wa albamu hiyo na pia Wateule.
Mojawapo ya nyimbo zilizomo katika albamu hiyo ni wimbo ambao unatamba katika vituo mbalimbali vya redio hivi sasa.Wimbo unaitwa Napenda Nini .Katika wimbo huu Jafarai ameshirikiana na mwanadada Fatma. Ni wimbo ambao una tungo kali,matata na ambayo nadhani ni huru kusema unaweza kuitafsiri unavyotaka wewe.Ni kazi nzuri ya sanaa ambayo inaonyesha jinsi gani lugha ya Kiswahili ni pana.Usikilize wimbo huo hapa chini na kisha jiulize; Jafarai Anapenda Nini?
Steven Kanumba gets Wema Sepetu Arrested
Wema Sepetu, the 2006 Miss Tanzania was arrested yesterday and charged with a charge of assault to actor Steven Kanumba as well as criminal damage to the actor's property. The former beauty queen is being held at a Magomeni Police cell in Dar-es-salaam. A friend close to Wema told SwahiliRemix.com that since Steven dumped Wema a few months ago, the heartbroken model and the film actor have been fighting each other whenever they meet. The pair who ended their on-off relationship last year were last seen in November spending quite a bit of time together.Our reporters efforts to reach the two through their mobiles has been fruitless. The family of Wema have been seen outside the police post trying to bail her out.
“TUGAWANE UMASIKINI” MAANA YAKE NINI?
Juma Nature ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao huathiri jamii moja kwa moja kila watoapo albamu au wimbo.Matumizi yake ya lugha,mtindo wake wa kughani au kurap,uhalisia wa kitu anachokiongelea nk ni miongoni mwa mambo ambayo yanamfanya atambe na akubalike zaidi.Hivi karibuni alitoa albamu ambayo ameipa jina la “Tugawane Umasikini”. Baada ya hapo kumekuwa na tafsiri mbalimbali kuhusu “kugawana umasikini”.Bila shaka umeshasikia mtu akikuambia ah…leo ni weekend bwana…ngoja tukagawane umasikini.Starehe mbalimbali zikiwemo ngono,pombe nk zimekuwa ni “kugawana umasikini”.Lakini yeye mwenyewe alikusudia au kumaanisha nini alipozungumzia “Kugawana Umasikini”? Ili kupata jibu kamili nilimtafuta Nature na kufanya naye mahojiano yafuatayo;
UHONDO:Mambo vipi Nature?Umeshamaliza tour ya kuzindua albamu yako?
NATURE: Mambo poa kabisa ndugu yangu.Tour naweza kusema bado inaendelea ingawa baada ya kutembelea mikoa kadhaa hivi sasa nimerejea nyumbani Dar kwa ajili ya mapumziko kidogo na kuangalia masuala ya familia.
UHONDO: Nimekutafuta kwa ajili ya kutaka kujua kitu kimoja; hivi karibuni umetoa albamu ambayo umeiita Tugawane Umasikini. Baada ya kutoka kwa albamu hiyo kumekuwepo na tafsiri mbalimbali kuhusu “kugawana umasikini”.Wengine wanasema kugawana umasikini ni pamoja na kugida maji kwa sana,ngono(zikiwemo zembe) na kwa ujumla kuamua tu kuishi bila kufanya kazi kwa juhudi kwa sababu tayari wengi wetu tu masikini na hivyo hakuna la kufanya.Je, wewe ulimaanisha nini haswa ulipotaka kuzungumzia “kugawana umasikini”?
NATURE: Ahahahaha, labda hapo naweza kusema hiyo ni kazi nzima ya fasihi kwamba kila mtu anaweza kuupokea ujumbe atakavyo au apendavyo na wote wakawa sahihi! Kimsingi nilichomaanisha ni kwamba kutokana na ukweli kwamba nchi yetu na wengi wa wanachi wake bado ni masikini, ni jambo muhimu sana kusaidiana.Pamoja na umasikini tulionao,endapo tutaamua kugawana hicho hicho kidogo tulichonacho basi kwa pamoja tutaweza kuinuana.Baba wa Taifa,Mwalimu Nyerere alipenda sana kutukumbusha kuhusu “Umoja ni Nguvu”.Hapo ndipo alipoongelea sana habari za Ujamaa na Kujitegemea.Leo hii tumesahau misingi ile na ndio maana labda tunaendelea kuwa masikini.Lakini mimi nikiwa nacho kidogo na nikamsaidia mwenzangu,basi kesho si ajabu na yeye akainuka na kumsaidia yule ama yule.Kwa mwendo huo tutafika mahali pazuri zaidi.Isitoshe hatuwezi kuzungumzia utajiri wakati sisi ni masikini.Hivyo ndivyo nilivyoomanisha na ndivyo nilivyokusudia.Wanaopotosha au kujaribu kupindisha maana halisi wanafanya hivyo kwa sababu zao wenyewe zikiwemo kujifariji nk. Lakini kama nilivyotangulia kusema hapo juu,hiyo ni kazi ya fasihi na hivyo siwezi kuwatolea macho au kuwalaumu.
UHONDO: Kama ulivyogusia katika jibu lako hapo juu,watanzania wengi bado ni masikini lakini pia wapo watu ambao ni matajiri wa kutupwa. Una ujumbe gani kwa matajiri hao?
NATURE: Ni kweli kabisa usemalo,wapo matajiri wa kutupwa.Ujumbe wangu kwao ni ule ule labda kwa mtindo tofauti kidogo tu.Badala ya kugawana umasikini wao nitawaambia wagawe utajiri walionao.Wakifanya hivyo nina uhakika wataendelea kuwa matajiri na pia kuinua hali za watu wengine.Umoja ni nguvu.
UHONDO: Kwa mtu ambaye anataka kununua albamu ya Tugawane Umasikini anaweza kuipata wapi?
NATURE: Albamu hivi sasa inapatikana kote mitaani.Lakini kwa uhakika anaweza kuipata pale Mamu Store-Kariakoo.Albamu hii inasambazwa na GMC Wasanii.
JK reaffirms free expression
President Jakaya Kikwete has reiterated the government’s commitment to guaranteeing freedom of opinion and expression, in order to strengthen democracy in contemporary Tanzania. President Kikwete said that Tanzania had since made positive inroads in its efforts to embrace all facets of democracy, including freedom of expression and opinion. The President, who is on a week-long working tour of the United States, made the remarks on Tuesday when he met Tanzanians living in Southern California.
Mr Kikwete said his government was also promoting key social values such as liberty, respect, harmony and tolerance, all of which would significantly contribute to peace and tranquillity in Tanzania. However, the president expressed concern over cases of abuse of these individual rights, saying freedom of expression and opinion are not the same thing as hurling insults or derogatory public utterances against other people.
But he expressed optimism that such outrageous tendencies would soon come to an end when people eventually build a culture of tolerance and political maturity. On dual citizenship, the president reiterated this was yet to be resolved and that “a significant number” of the local population back home was still against it. Meanwhile, the president has called on Tanzanians in the Diaspora – yet again to support the country’s collective development effort -- as a means of improving the living standards in their mother country.
Mr Kikwete was addressing another ‘meet-the-president’ session with Tanzanians living abroad, the same at the Beverly Hills Hilton – also in Los Angeles. He stressed the need for all those living abroad to plough back recourse at home – even as they help to provide assistance to the needy and their own relatives. The president also outlined a catalogue of achievements made during his office so far, especially in social and physical infrastructural developments.
Subscribe to:
Posts (Atom)